Thursday, August 16, 2007

WITO WA MKUTANO WA WAZAZI

WITO WA MKUTANO WA WAZAZI WA
JITEGEMEE SEKONDARI KIDATO CHA I-VI
TAREHE 18 AUG 2007
1. Katika utaratibu wetu tuliojipangia wa kuongea na wazazi/walezi wa wanafunzi juu ya mikakati ya kuboresha elimu katika kufundisha na kujifunza,ninayo heshima kukufahamisha kwamba unaalikwa kwenye mkutano wa wazazi/walezi na walimu wa wanafunzi wa shule hii utakaofanyika Jumamosi tarehe 18 Aug 2007 kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana katika Ukumbi wa Maafisa Mgulani JKT.
2. Aidha, ukiwa kama mzazi/mlezi tunaomba ufike mapema saa 2.00 asubuhi ili uweze kupata fursa ya kubadilishana mawazo na mwalimu wa darasa juu ya mwenendo wa kitaaluma na nidhamu ya mtoto wako.
3. Unaombwa kujali muda, na kuhudhuria bila kukosa.Mpango huu ni muhimu sana.Lengo ni kupanga mkakati wa pamoja kwa manufaa ya watoto wetu
Wasalamu,
(ME Mkisi)
Mkuu wa Shule.

No comments: